Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: tovuti ya A.B.C Australia imetangaza kuwa gaidi maarufu wa Australia (Nail Parakash) ameangamia katika mashambulizi yaliofanyika katika mkoa wa Mosul nchini Iraq.
Gaidi huyo alikuwa anatuhumiwa kupanga mashambulizi kadhaa ya kigaidi nchini Australia na kutaka kufanya mauaji hayo kwa njia ya mtu binafsi.
Mashambulio ya mtu binafsi ni kwamba kila gaidi mmoja yeye pekee ndiye atakaye panga jinsi ya kufanya mashambulizi ya hayo bila ya kushirikiana kimawasiliano na yeyote yule, kwa lengo la kupoteza ushaidi kuwa anamahusiano na kikundi chochote cha kigaidi, hivyo kufanya hali uchunguzi kuwa mzito kwa vyombo vya ulnzi na usalama.
Gaidi huyo ambaye ni maarufu kwa lakabu ya Abu Khalidi Cambojiy ambaye ameangamia katika mkoa wa Mosul nchini Iraq, aliondoka nchini Australia mwaka 2013 na kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Gaidi huyo alituhumiwa kupanga mashambulizi ya siku ya Anzac mwaka uliopita, siku ya Anzac ni siku iliowekwa kwaajili ya jeshi la Australia na New Zealand ambapo walishirikiana katika vita ya kwanza ya dunia wakiisaidiA Uingereza.
Gaidi huyo pia alionekana mwaka jana katika filamo za matangazo ya kikundi cha kigaidi cha Daesh huku akitangaza kufanya mashambuliz ya kigaidi nchini Australia.
mwisho wa Habari/290